UPENDO WA BABA NA MAMA

Salaam kwako baba, Nakusalimia baba,
Mimi Ali Muya baba, Nipe yangu marahaba,
Baraka nitie baba, Moyo wangu uwe shaba,
Kwako hayo yako mahaba, Leo nimekuwa baba.

Leo hii ni mzima, Asante apewe Mungu,
Leo hii niko wima, Sifa zote zako Mungu,
Kukuabudu lazima, Kutimiza langu fungu,
Naomba zako rehema, Niepuke na majungu.

Baba kwa mara ya kwanza, Ulinipa zangu raba,
Nikaingia la kwanza, Nikamaliza la saba,
Sekondari nikaqnza, Nikasoma maktaba,
Kwa hayo yako mahaba, Leo nimekuwa baba.

Alipokuwepo mama, Mungu ampe rehema,
Alinifunza heshima, Kuifahamu hekima,
Bila upendo wa mama, Leo nisingesimama,
Nimekukumbuka mama, Leo nimekuwa baba.

Pendo la baba na mama, Hakuna kinachokwama,
Likiniponda diaba, Mama apata lawama,
Baba akiwa mraba, Sifa huzipata mama,
Watii mama na baba, Utapata usalama.

Utaipata neema, Utaona nilosema,
Ukifanya wako wema, Utavuna yote mema,
Mwanadamu hana jema, Ufanyalo watasema,
Mama na baba ni hema, Ukiwakosa yatima.

This poem is about: 
My community

Comments

Additional Resources

Get AI Feedback on your poem

Interested in feedback on your poem? Try our AI Feedback tool.
 

 

If You Need Support

If you ever need help or support, we trust CrisisTextline.org for people dealing with depression. Text HOME to 741741