KIDATO CHA NNE

Enyi kidato cha nne, huu ni mwaka mwengine,
Zitafuteni A nne, tuko sheria nyingine,
Msitafute D nne, kama miaka mingine,
Hebu mshirikiane, pia msaidiane.

Njia yenu ya mwanzoni, darasa lile la nne,
Njia yenu ya mtoni, kumi kenda toa nne,
Njia ile ya mtoni, cha pili kabla cha nne,
Kidato hiki cha nne, ni njia yenu ya nne.

Kidato chenu cha nne, si kama njia zingine,
Hii ina pembe nne, yenye milango minne,
Ukifungua mwengine, hautavuna minne,
Utasahau vingine, wanajutia wengine.

Huu mlango wa nne, wenye sifa zake nne,
Kuziona sifa nne, tofauti na zengine,
Kufahamu hizo nne, njooni mwaka mwengine,
Ntasema zote nne, hata mikiwa wa nne.

Nimemalizq wa nne, huu ubeti mwengine,
Sisemi hayo mengine, waongee na wengine,
Mi mtoto wa Mwanne, nataka muungane.

Comments

Additional Resources

Get AI Feedback on your poem

Interested in feedback on your poem? Try our AI Feedback tool.
 

 

If You Need Support

If you ever need help or support, we trust CrisisTextline.org for people dealing with depression. Text HOME to 741741