KIBERITI
Kiberiti kiloshika, Sasa kimeharibika,
Cha baki kuhangaika, Njiti zazidi chomoka,
Umoja ulioshika, Umezidi kuponyoka,
Upendo ulisikika, Umekwisha ondoka.
Njiti kwanza ikitoka, Huenda kuburudika,
Ganda hubadilika, Na kuanza kukwaruzika,
Ganda hukasirika, Na moto waja kuzuka,
Njiti huangaika, Hadi kumumunyuka.
Halufu ikisikika, Njiti wa pili hutoka,
Huja kwanza kuruka, Ili Ganda kumshika,
Pale anaposhuka, Moto huja kuwaka,
Njiti hushika, Na majivu hutoka.
Mtu akifika, Hakuna wa kuchomoka,
Hata waliosalimika, Hawawezi kutoroka,
Mtu njiti hushika, Na Ganda kutikisika,
Moto ukishika, Wote huharibika.